MKUU wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack, amefungua Mafunzo yenye kulenga kuwaelimisha wajasilimali ambao ni wasindikaji na wafungashaji wa Korosho na bidhaa za korosho zinazozalishwa katika mkoa huo.
Akizungumza katika Mafunzo hayo yaliyo ratibiwa na TBS, Telack amesema Mafunzo ni njia muafaka ya kuleta tija katika juhudi za kuliletea taifa maendeleo ya haraka kulingana na fursa zilizopo hasa kwenye sekta ya Viwanda, Kilimo, Biashara na maeneo mengine.
RC Telack amesema Serikali imeazimia kwa dhati kuendeleza Viwanda ili kutoa ajira katika Kada mbalimbali pamoja na kuziwezesha bidhaa kushindana katika masoko ya ndani kikanda na nje ya Tanzania.
Aidha, RC Telack ameipongeza TBS kwa kusimamia mafunzo hayo huku akiwataka waendeleze majukumu hayo kwa kushirikiana na watendaji waliopo kwenye halmashauri zote nchini ili kuweza kurahisisha kufikisha huduma kwa wananchi.
Na Sophia Nyalusi, Lindi