HOSPITALI ya Kanda ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, imeanza kutoa matibabu ya kurudisha Utumbo ndani ya Tumbo kwa watoto wanaozaliwa na tatizo hilo.
Daktari wa Kitengo cha Watoto, Dokta Kahabi William ameelezeahatua hiyo wakati wa maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Hospitali hiyo yanayoendelea jijini Mwanza.
Matibabu hayo yalianza Juni mwaka huu baada ya kupatikana kwa vifaa hasa Mfuko maalumu wa kurudisha Utumbo ndani ya Tumbo.
Awali watoto walikua wakifariki Dunia kutokana na uhaba wa vifaa unaotokana na gharama kuwa juu, ambayo si chini ya Shilingi laki tisa kwa mfuko.
Kwa mujibu wa Dokta Kahabi, chanzo cha tatizo hilo bado hakijajulikana lakini Wajawazito wanashauriwa kufanya kipimo cha kuchunguza maendeleo ya Mtoto Tumboni ili kubaini matatizo na kujiandaa kukabiliana nayo kwa wakati.
Na MWANDISHI WETU