CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, mkoani Arusha William Tate Ole Nasha, kilichotokea Septemba 27, 2021 nyumbani kwake jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema William Ole Nasha alikuwa kiongozi muaminifu na mzalendo ambaye wakati wote alijutuma kwa bidi na juhudi katika ujenzi wa nchi.