MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam-DAWASA imewatoa hofu wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuwa hakuna mwananchi atakayekosa huduma ya Maji kipindi hiki cha upungufu wa Maji katika Bonde la Mto Ruvu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema Mamlaka kwa kushirikiana na Bonde la Ruvu wanaendelea kuhakikisha vibali vya watumiaji wengine wa Maji ikiwa ni pamoja na Wafugaji na Wakulima vinasitishwa ili kuongeza zaidi kina cha Maji katika Bonde hilo.
Na MWANDISHI WETU