MKUU wa Wilaya ya Muheza, Halima Bulembo, ameiomba Serikali kuipa kipaumbele barabara ya Amani Muheza kwa kile alichodai barabara hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya Wilaya hiyo.
Halima alitoa ombi hilo wakati wa Ziara ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa, alipofika Wilayani hapo kwa lengo la kukagua maendeleo ya Mradi huo.
Amesema Barabara hiyo ndio kiungo kikuu na kwamba inatumika na wakulima wa mazao ya Iriki pamoja na vivutio vya utalii ambavyo vinapatikana Wilani humo katika eneo la Amani.
‘Mhe. Waziri Nakuomba utufikishie salamu zetu kwa Rais Samia kwamba tunamshuku kwa Mradi huu maana tunaamini ukikamilika utakuza kipato cha wananchi wa Muheza lakini pia kwa Taifa letu ” amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
Ameongeza kuwa eneo la amani linategemewa sana kwa kilimo cha Viungo, vivutio vya utalii pamoja na vyanzo vya maji ambapo wananchi wengi wa muheza hutumia barabara hiyo kwa ajili ya shughuli zao za kila siku.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Prof. Mbarawa amemesema Mradi mpaka sasa umefikia asilimia 93 na kwamba Serikali tayari imekwisha tenga fedha kwa ajili ya kukamilisha Mradi huo.
Suzan Uhinga Tanga.