DEREVA Paul Vedastus (33) maarufu Majani, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha pili.
Majani aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka mawili la kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi, alipewa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na la kumbaka kifungo cha miaka 30, hata hivyo adhabu hizo zinaenda pamoja, hivyo atatumikia kifungo cha miaka 30.
Majani amepewa adhabu hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati shauri linalomkabili lilipopelekwa kwa kutolewa hukumu.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Simba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati shauri hilo lilipopelekwa kwa hukumu.
Hakimu Simba alisema wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi watano, waliothibitisha mashitaka dhidi ya mshitakiwa pasi na kuacha shaka yoyote.
Hakimu Simba alifafanua kuwa katika uchambuzi wa mashahidi hao akiwemo shahidi wa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aliyechukua vipimo vya vinasaba kutoka kwa mtoto aliyezaliwa na mwanafunzi huyo(jina linahifadhiwa) na mshitakiwa, alithibitisha kwamba ni baba wa mtoto huyo.
“Mtendewa alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili mwaka 2016 na akiwa na umri wa miaka 16 na alijifungua mtoto, ambapo shahidi wa tano alimpima vipimo 15 vilivyothibitisha mshitakiwa ndiye baba wa mtoto kwa asilimia 99.9,” alisema.
Hakimu Simba alisema kwa uthibitisho huo uliotolewa mahakamani, mshitakiwa anamtia hatiani kama alivyoshitakiwa, ambapo katika kosa la kwanza la kumpa mwanafunzi ujauzito anamhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na la pili kifungo cha miaka 30 jela.
Hata hivyo, Hakimu Simba alisema adhabu hizo za kifungo zinakwenda pamoja, hivyo mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30.
Pia, alisema katika shtaka la pili la ubakaji, anamhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, ambapo adhabu hiyo inakwenda kwa pamoja, hivyo atatumikia kifungo cha miaka 30 jela.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai hana kumbukumbu ya nyuma ya makosa ya mshitakiwa, hivyo aliomba Mahakama kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wa mshitakiwa, aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana familia ambayo inamtegemea ya watoto watatu na wazazi wake ni wagonjwa.
Baada ya kudai hayo, Hakimu Simba alisema adhabu ya makosa kama hayo yamepangwa kwa mujibu wa sheria, kwasababu wanafunzi wanapewa ujauzito, hivyo adhabu hiyo iko kwa mujibu wa sheria hakuna namna ya kuibadilisha ni miaka 30 jela kila kosa
Hakimu Simba alitoa amri ya kumrudishia mlalamikaji cheti chake za kuzaliwa. Mshitakiwa alitenda kosa hilo, kati ya Mei na Agosti, mwaka 2016, eneo la Tandika wilayani Temeke, Dar es Salaam. Mshitakiwa huyo siku hiyo na maeneo hayo alimbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi huyo.
MARIAM MAWAZO (DMC) Na SYLVIA SEBASTIAN