RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi ambapo ameingiza mawaziri wapya wanne na naibu mawaziri saba.
Aidha, ameigawa iliyokuwa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto kuwa wizara mbili huku akiwabadilisha wizara baadhi ya mawaziri.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulku Zanzibar, Mhandisi Zena Saidi ilisema kuwa, mawaziri na naibu mawaziri hao wataapishwa kesho.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Baraza la Mapinduzi Zanzibar sasa litakuwa na wizara na naibu mawaziri wake kwenye mabano kama ifuatavyo:
OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu (Jamal Kassim Ali), kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ (Masoud Ali Mohammed).
Ilisema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (Haroun Ali Suleiman), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji (Mudrik Ramadhan Soraga) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango (Dk. Saada Mkuya Salum) ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
(Harusi Said Suleiman).
OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi – Hamza Hassan Juma).
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, waziri ni (Dk. Khalid Salum Mohamed) ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi.
Ilisema Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo (Shamata Shaame Khamis), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali (Lela Muhamed Mussa) ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.
Wengine ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (Tabia Maulid Mwita), Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (Rahma Kassim Ali) ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.
Mwaziri wengine ni Waziri wa Maji, Nishati na Madini (Shaib Hassan Kaduara), Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi (Suleiman Masoud Makame) ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini.
Iliwataja mawaziri wengine ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale (Simai Mohamed Said), ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Waziri wa Afya (Nassor Ahmed Mazrui) na kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.
Aidha, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(Riziki Pembe Juma), kabla ya hapo alikuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda (Omar Said Shaaban).
NAIBU MAWAZIRI:
Kwa upande wa manaibu waziri ni Ali Suleiman Ameir ‘Mrembo’ (Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango), Juma Makungu Juma (Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi) na Ali Abdulgullam Hussein (Elimu na Mafunzo ya Amali).
Wengine ni Hassan Khamis Hafidh (Afya), Anna Athanas Paul (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto), Shaaban Ali Othman (Maji, Nishati na Madini) na Nadir Abdullatif Yussuf Alwardy (Ardhi na Maendeleo ya Makaazi).
Taarifa hiyo ilisema uteuzi huo ulianzia jana na kwamba mawaziri wapya na wale waliobadilishiwa wizara, pamoja na naibu mawaziri wataapishwa Ikulu kuanzia saa 3.00 asubuhi.
Na MWANDISHI WETU