RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amefanya uteuzi wa viongozi wanane katika taasisi mbalimbali, akiwemo Hassan Simba Hassan, aliyemteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Kurusha Maudhui.
Pia, amewateua Mwalimu Ali Mwalimu, kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BTMZ) na Omar Salum Mohamed, kuwa Kamishna wa Utamaduni katika Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said ilieleza kuwa Rais Mwinyi amemteua Hiji Dadi Shajak, kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Kurusha Mahudhui (ZMUX).
Vilevile Rais Dk. Mwinyi alimeteua Suleiman Abdulla Salim, kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji na Ali Haji Mwadini kuwa Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amemteua Robert Laurian Mweiro kuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Mifumo ya Tehama katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.
Pia, Rais Dk. Mwinyi amemteua Ali Khamis Mohamed kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mjini Unguja.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi ametengua uteuzi wa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Zanzibar, Mhandisi Fauzia Sinde Hassan kuanzia Septemba 28, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo uteuzi wa viongozi hao ulianza jana.
Na MWANDISHI WETU