NAIBU SPIKA wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Tulia Ackson afanya Ziara katika Kampuni ya Startimes jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya kutembelea Kampuni hiyo ya Startimes limited Makao makuu Bamaga jijini Dar es salaam amewapongeza kutokana na utoaji wao wa ajira kwa vijana wengi.
“Imekua moja ya Kampuni ambayo inatoa ajira kwa vijana hasaa ajira ya kudumu kwa vijana 500 na kwa upande wa mauzo sehemu mbalimbali imetoa ajira kwa vijana elfu 2000 hivyo kwa jinsi gani utaona ni Kampuni ambayo ipo sio kwa lengo tu la kujinufaisha yenyewe bali ipo kwa kuunga Mkono Serikali ya awamu ya 5 chini ya Rais wetu mpendwa Mama Samia Hassan Suluhu kuwezesha upatikanaji wa ajira hasa Kwa vijana,” amesema Dk. Tulia
Pia Tulia amewapongeza kwa uwekezaji Mkubwa kwa Kampuni ya Startimes na kuhakikisha inawezesha Watanzania wanapata vitu mbalimbali kupitia King’amuzi cha Startimes kutokana na kutoa kwao Maudhui mbalimbali ya kiburudani hususani tamthilia na filamu zenye kutumia lugha ya kiswahili.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malisa amesema ujio wa Naibu Waziri utaleta chachu na maboresho mbalimbali katika Kampuni hiyo ili kuleta Mabadiliko katika tasnia ya Burudani.
“Ujio wake ni wa Baraka Sana kwa siku ya Leo sote tunatambua umuhimu wa kiongozi wetu Mchapakazi ambae anashirikiana na vijana vizuri hivyo kwa siku ya Leo ametupa mwanga kwa namna gani tutaweza kuendesha Kampuni yetu.” amesema Malisa
Hata hivyo Malisa ameeleza kiundani zaidi Ushauri ambao umetolewa na kiongozi juu ya Kuboresha Maudhui hasa ya Kimichezo katika Tv3ambayo ni mpya.
“Kama tunavojua Dk.Tulia anapenda Michezo hivyo ametusihi tuongeze vipindi vya Michezo kwa wanawake hasa Netball na rede ikiwezakana iwepo na Michuano kwa ajili ya wanawake zaidi ili waweze kupewa nafasi katika jamii.” Malisa
Na AMINA KASHEBA