WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ameagiza kukamatwa watu 51 waliofanya utapeli kwa kuwauzia watu 206 viwanja maeneo ambayo yana hati za viwanda na hivyo kuonekana wavamizi.
Pia, ameagiza waliojenga bila vibali katika Jiji la Dodoma wawekewe alama nyekundu ya X huku Mtendaji wa Mtaa wa M’buyuni, Victoria Mzava, katika Kata ya Kizota akitakiwa kuchunguzwa kwa madai ya kuidhinisha malipo ya ununuzi ardhi kwa thamani ya Tsh. milioni 80 yaliyoratibiwa na Mtendaji aliyepita.
Waziri Lukuvi ametoa maelekezo hayo wakati akikabidhi taarifa ya uchunguzi uliofanywa na timu, aliyounda Februari 6 mwaka huu, wakati alipofika eneo hilo kusikiliza changamoto ya mgogoro wa ardhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, RC Mtaka amemhakikishia Waziri Lukuvi, kuwa yaliyomo ndani ya ripoti hiyo yatafanyiwa kazi na atashughulika na watakaobainika kuendelea kufanya utapeli wa aina hiyo.
Na SELINA MATHEW, Dodoma