Saturday, August 13, 2022
27 °c
Dar es Salaam
25 ° Thu
25 ° Fri
25 ° Sat
25 ° Sun
25 ° Mon
English EN Kiswahili SW
UHURU MEDIA GROUP
Tangaza Nasi
  • Mwanzo
  • Siasa
    • All
    • Business
    MEMBE ATOA YA MOYONI AKIREJEA CCM

    MEMBE ATOA YA MOYONI AKIREJEA CCM

    SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

    NI HISTORIA NYINGINE CCM

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM ITAENDELEA KUWA CHAMA BORA, IMARA AFRIKA- SHAKA

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
  • Michezo
    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    PABLO AIPANIA KMC 

    PABLO AIPANIA KMC 

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • UMG
    • Home
    • About Us
    • Services
    • Shop
    • Contact Us
  • MAGAZETI
    • Uhuru wanawake
    • Mzalendo
    • Uhuru vijijini
    • Burudani
    • Uhuru kijani
  • UHURU FM
    • Ratiba
  • UHURU DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • Mwanzo
  • Siasa
    • All
    • Business
    MEMBE ATOA YA MOYONI AKIREJEA CCM

    MEMBE ATOA YA MOYONI AKIREJEA CCM

    SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

    NI HISTORIA NYINGINE CCM

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM ITAENDELEA KUWA CHAMA BORA, IMARA AFRIKA- SHAKA

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
  • Michezo
    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    PABLO AIPANIA KMC 

    PABLO AIPANIA KMC 

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
No Result
View All Result
UHURU MEDIA GROUP
No Result
View All Result
Mwanzo MAKALA AFYA

MABORESHO IDARA YA UUGUZI, UKUNGA YANACHOCHEA HUDUMA BORA ZA AFYA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 8, 2021
in MAKALA AFYA
0 0
0
MABORESHO IDARA YA UUGUZI, UKUNGA YANACHOCHEA HUDUMA BORA ZA AFYA

WAZIRI wa afya Dk.Gwajima akizungumza baada ya kuzindua Baraza la Uuguzi na Wakunga hivi karibuni Mkoani Pwani

0
SHARES
225
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

UUGUZI na ukunga ni muhimu katika kupunguza maumivu kwa wagonjwa, kuboresha huduma ya mama na mtoto na makundi mengine ndani ya jamii.

Kutokana na umuhimu huo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dk.Dorothy Gwajima akizindua  Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), anasema baraza hilo  lina wajibu wa kuhakikisha linalinda, kuimarisha na kuhifadhi afya ya jamii, usalama na ustawi, kupitia usimamizi na udhibiti wa shughuli za mafunzo ya uuguzi na ukunga.

“Wahitimu wamekuwa wengi na hawana stadi za kutosha, kumekuwa na utitiri wa vyuo na havina vigezo vya  kutosha  katika maeneo ambayo hayakidhi vigezo, vifaa kama serikali tutashughulika navyo,wale wanaosoma vyuo ambavyo havijasajiliwa wanajifurahisha  maana hawatasajiliwa,”anasema.

Dk.Gwajima anasema, takribani asilimia 60 ya watoa huduma za afya nchini ni wauguzi na wakunga, ikilinganishwa na kada zingine.

“Tasnia hii inafanya kazi ya wataalamu wengine pale wapokuwa hawapo, unakuta wauguzi wanawapa wagonjwa dawa, wanakaa na watoto na kwa uzoefu wake unamhudumia mgonjwa, hivyo tunakila sababu ya kuwasaidia,’’anasema.

Dk.Gwajima anabainisha kuwa, ili kuboresha huduma inayotolewa na wakunga na wauguzi, ni muhimu TNMC kuandaa miongozo ya kutolea huduma na zipatikane mahala pa kazi.

“Hakikisheni miongozo hii inapatikana katika maeneo ya kutolea huduma na iwe rahisi mtu kuipata mitandaoni.

Kwa upande wa serikali, tutakwenda kuhakikisha tunaimarisha uwepo wa wauguzi katika vyombo vya maamuzi, kazi  hii ni kubwa ya kusimamia  na kutetea maslahi ya wauguzi kupitia sheria,”anaseama.

MAGEUZI KWA WAUGUZI,WAKUNGA

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya Ziada Sellah, akizungumzia maendeleo ya fani hiyo anasema, miaka ya nyuma wauguzi walikuwa wakiishia kupata mafunzo ngazi ya cheti na stashahada.

“Walikuwa hawapati mafunzo zaidi, baada ya kuona dunia inakimbia  kwa kasi, tukaona na sisi Tanzania tunatakiwa kwenda kasi ndipo ikaanzishwa  mafunzo ngazi ya shahada na wauguzi wengi wakaanza kufikia ngazi hiyo.

Tulianza kufika mbali zaidi na wauguzi na wakunga wakawa wanapata elimu ngazi ya uzamili

Hadi sasa ukiangalia tuna wauguzi wengi ambao wana shahada ya uzamivu, ambao wana uwezo wa kuchapisha maandiko,”anasema.

Ziada anasema katika fani ya uuguzi na ukunga wapo waliobobea.

MKURUGENZ wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Ziada Sellah

Kwa upande wa changamoto Ziada anasema, vyuo vimekuwa vikiongezeka bila kuwa na udhibiti  hali inayochangia wauguzi wanaohitimu kukosa ubora.

“Vikidhibitiwa unajua kabisa muuguzi au mkunga anayemaliza mafunzo anasifa zinazostahili kuwa katika fani hiyo.

Tunaamini tukikaa chini na kukabaliana na utitiri wa vyuo tutapunguza idadi ya wauguzi wasio na sifa  na kuzalisha wenye ujuzi na stadi,”anasema.

Ziada anataja changamoto nyingine kuwa ni malamiko katika jamii  yanayotokana na wauguzi na wakunga kukosa maadili.

Anasema, TNMC ina ukosefu wa fedha hivyo baraza lililozinduliwa linajukumu la kuhakikisha TNMC inapata rasilimali fedha, kutekeleza majukumu yake mbalimbali.

“Wananchi inayoikabili baraza  ni wananchi kutofahamu kazi ya muuguzi na mkunga,”anasema..

Akizungumzia ukaguzi wa matibabu Ziada anasema, utaisaidia TNMC kuangalia ukaguzi wa kimatibabu.

“Tunakwenda kuangalia mkunga kafanya nini  na mwisho wa siku tunagundua changamoto iko wapi.

Kuna dawati tumelianzisha linaloangalia huduma ambayo inajali utu   heshima na maadili ya ukunga na uguzi, kila mgojwa anayekuja   anahitaji kutambulika na  anatakiwa kupata huduma  bila kuwagawa katika makundi,’’anasema.

Ziada anasema,TNMC itahakikisha maadili ya wauguzi hayaendi nje ya maadili.

“Ili uwe muuguzi au mkunga ni lazima uwe na maadili yanayokufanya ufanye kazi,’’anasema.

Katika udhibiti wa ugonjwa wa Corona, Ziada anasema siku zote wapo mstari wa mbele na ndio wa kwanza katika udhibiti wa ugonjwa huo.

“Muuguzi anakuhudumia saa 24 siku saba katika wiki, ukiingia hospitali unakutana na muuguzi wa kwanza, ukilazwa unakuwa na muuguzi ukiruhusiwa  upo na  muuguzi

Kuhusu janga la corona sisi tuna nafasi kubwa kuhakikisha tunampa  huduma mgojwa kulingana na changamoto alizonazo, daktari atakuja kwa ajili ya ushauri  na kukuandikia dawa.

Muuguzi ndiye atakaye kujali, ana nafasi ya kutoa elimu kwa jamii kwani ni kazi yake kubwa kwa hiyo hii ni nafasi yetu kubwa,’’anasema.

Miaka mitatu ya TNMC, miongoni mwa mambo ya kujivunia ni wauguzi na wakunga walio hitimu katika vyuo mbalimbali kuidhinishwa.

Wauguzi na wakunga 8,983 wamesajiliwa  na kupewa leseni, huku vyuo  vipya vya uuguzi na ukunga vitatu  vikianzishwa na 25 vikipanda kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya astashahada hadi stsshahada.

Vilevile kwa mujibu wa TNMC vituo binafsi vya uuguzi na ukunga vitano viliidhinishwa

Mbali na hayo TNMC imesimamia matumizi  bora ya taasisi na kuwachukulia hatua watumishi wasiofuata maadili, ambapo jumla ya watuhumiwa saba walifuatiliwa na kutiwa hatiani.

Pia baraza limeboresha kanzidata, ambapo wauguzi na wakunga wanapata huduma kwa njia ya mtandao.

BARAZA LA UUGUZI,UKUNGA

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Wakunga Agnes Mtawa, anasema  baraza hilo lilianzishwa mwaka 1953, chini ya sheria ya usajili uuguzi na ukunga

“Sheria hiyo ikafanyiwa marekebisho mwaka 1997 na mwaka 2010, sasa baraza linafanya kazi chini ya sheria namba moja ya mwaka 2010, ambayo imefanyiwa maboresho na kuifanya taaluma hii  ikuwe.

MUUGUZI akitoa huduma ya afya kwa mgonjwa

Baraza lilipata hadhi ya kuwa taasisi mwaka 2014 na tangu hapo  limetekeleza miongozo ya watoa taaluma kutoa huduma  za uuguzi na ukunga.

Tayari tumeshatengeneza muundo na mfumo wa usajili ambapo idadi ya waguzi na wakunga kwa sasa ni rahisi kufahamika, tumetengeneza miongozo inayolenga kuboresha huduma za uuguzi na wakunga.

Agnes anasema hadi sasa wauguzi na wakunga waliopo nchini ni 46,000  huku TNMC ikiwa na mkakati wa miaka mitano ambao ndio muongozo wa kutoa huduma za uuguzi na ukunga yenye kufanya baraza hilo kusonga mbele,’

“Baraza lipo kuhakikisha jamii inapata huduma bora kwa kutatua changamoto, wanachama na watoa  huduma wafuate sheria,”anasema.

Ili kuboresha huduma ya uuguzi na ukunga, Isaya Jacob anasema  kufanyike uchunguzi ili wauguzi na wakunga wasio na sifa walio katika vituo vya afya waondolewe.

 

Abdurahman Jumanne

Abdurahman Jumanne

Stay Connected test

  • 116 Follower
  • 172k Subscriber
  • 23.6k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
MBUNGE LINDI ATAKA VIJANA WAJISHUGHULISHE

MBUNGE LINDI ATAKA VIJANA WAJISHUGHULISHE

July 8, 2021
NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

0
WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

0

OFISA ELIMU, MHANDISI, MKUU WA SHULE WAKALIA ‘KUTI KAVU’

0
STENDI YA ZAMANI UBUNGO  KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

STENDI YA ZAMANI UBUNGO KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

0
MIAKA 30 YA VYAMA VINGI: CHANGAMOTO NA MUSTAKABALI KUSONGA MBELE

MIAKA 30 YA VYAMA VINGI: CHANGAMOTO NA MUSTAKABALI KUSONGA MBELE

July 1, 2022
WAWILI WADAKWA DAR TUHUMA ZA BIASHARA YA NGONO MTANDAONI

WAWILI WADAKWA DAR TUHUMA ZA BIASHARA YA NGONO MTANDAONI

June 28, 2022
WAJUE WATIKISA NYAVU BORA 2021/2022

WAJUE WATIKISA NYAVU BORA 2021/2022

June 28, 2022
ATOZWA FAINI 100,000 KISA KUIBA PUNDA WA BABA YAKE

ATOZWA FAINI 100,000 KISA KUIBA PUNDA WA BABA YAKE

June 28, 2022

Recent News

MIAKA 30 YA VYAMA VINGI: CHANGAMOTO NA MUSTAKABALI KUSONGA MBELE

MIAKA 30 YA VYAMA VINGI: CHANGAMOTO NA MUSTAKABALI KUSONGA MBELE

July 1, 2022
WAWILI WADAKWA DAR TUHUMA ZA BIASHARA YA NGONO MTANDAONI

WAWILI WADAKWA DAR TUHUMA ZA BIASHARA YA NGONO MTANDAONI

June 28, 2022
WAJUE WATIKISA NYAVU BORA 2021/2022

WAJUE WATIKISA NYAVU BORA 2021/2022

June 28, 2022
ATOZWA FAINI 100,000 KISA KUIBA PUNDA WA BABA YAKE

ATOZWA FAINI 100,000 KISA KUIBA PUNDA WA BABA YAKE

June 28, 2022
Instagram Youtube Twitter Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • 2021
  • Afya Makala
  • BURUDANI
  • Business
  • GAZETI LA BURUDANI
  • GAZETI LA UHURU
  • GAZETI LA UHURU MACHI 17
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • KIMATAIFA
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • RIWAYA
  • SIASA
  • Uncategorized

Recent News

MIAKA 30 YA VYAMA VINGI: CHANGAMOTO NA MUSTAKABALI KUSONGA MBELE

MIAKA 30 YA VYAMA VINGI: CHANGAMOTO NA MUSTAKABALI KUSONGA MBELE

July 1, 2022
WAWILI WADAKWA DAR TUHUMA ZA BIASHARA YA NGONO MTANDAONI

WAWILI WADAKWA DAR TUHUMA ZA BIASHARA YA NGONO MTANDAONI

June 28, 2022

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In