Saturday, May 21, 2022
27 °c
Dar es Salaam
25 ° Thu
25 ° Fri
25 ° Sat
25 ° Sun
25 ° Mon
English EN Kiswahili SW
UHURU MEDIA GROUP
Tangaza Nasi
  • Mwanzo
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

    NI HISTORIA NYINGINE CCM

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM ITAENDELEA KUWA CHAMA BORA, IMARA AFRIKA- SHAKA

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
  • Michezo
    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    PABLO AIPANIA KMC 

    PABLO AIPANIA KMC 

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • UMG
    • Home
    • About Us
    • Services
    • Shop
    • Contact Us
  • MAGAZETI
    • Uhuru wanawake
    • Mzalendo
    • Uhuru vijijini
    • Burudani
    • Uhuru kijani
  • UHURU FM
    • Ratiba
  • UHURU DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • Mwanzo
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

    NI HISTORIA NYINGINE CCM

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM ITAENDELEA KUWA CHAMA BORA, IMARA AFRIKA- SHAKA

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
  • Michezo
    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    PABLO AIPANIA KMC 

    PABLO AIPANIA KMC 

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
No Result
View All Result
UHURU MEDIA GROUP
No Result
View All Result
Mwanzo Habari Kitaifa

MAJALIWA APOKEA MAJINA 453 WALIO TAYARI KUHAMA NGORONGORO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 11, 2022
in Habari Kitaifa
0 0
0
MAJALIWA APOKEA MAJINA 453 WALIO TAYARI KUHAMA NGORONGORO

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453.

0
SHARES
42
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amepokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye Hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari yao huku wengine wakiendelea kujiandikisha.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mazungumzo ambayo Waziri Mkuu aliyafanya na wadau wa uhifadhi kwenye vikao vilivyofanyika Februari 14 na 17, mwaka huu kwenye Tarafa za Loliondo na Ngorongoro, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

Waziri Mkuu alipokea majina hayo baada ya kumaliza kikao na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanan) kwenye mkutano uliofanyika eneo la Oretei Loongaik – Marya, kwenye Chuo cha Ufundi Arusha, jijini Arusha. Eneo hilo hufanyika bunge la viongozi hao na hutumika pia kufanyia ibada za kimila.

Akikabidhi orodha hiyo kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, alisema majina hayo ni ya awali na tayari yalishahakikiwa mara baada ya wakazi hao kujiandikisha. “Tutawasimamia vizuri hadi waende kule wapate hati za mashamba, nyumba na maeneo ya kulisha mifugo yao.”

Akizungumza na Malaigwanan hao zaidi ya 350, Waziri Mkuu alisema Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara mkoani humo aliliambia taifa iko hatari ya kutoweka kwa Hifadhi ya Ngorongoro ndani ya muda mfupi na akatoa maagizo viongozi waende kuwasikiliza wananchi juu ya hatua za kuchukua ili tunu hiyo isipotee.

“Ile hatari aliyosema Rais ni ipi? Zamani watu waliweza kuishi na wanyama bila tatizo kwa sababu kulikuwa na wakazi 8,000 tu wenye ng’ombe 20 hadi 30. Leo hii kuna wakazi 110,000 na mifugo zaidi ya 813,000 wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo.

Aliwaeleza viongozi hao kwamba serikali imetenga eneo la kilometa za mraba 400,000 wilayani Handeni ambalo kati ya hizo, kilometa za mraba 220,000 zilitumika kwa kujenga nyumba, kupima viwanja na kutenga maeneo ya malisho.

“Tumepima viwanja 2,406 ambapo kati ya hivyo, viwanja 2,070 tumeandaa kwa ajili ya makazi na kila kimoja kina ukubwa wa ekari tatu. Tumeanza na nyumba za kuanzia 101 za vyumba vitatu vya kulala kwa wale wanaotaka. Tuna viwanja 336 kwa ajili ya huduma kama shule za msingi na sekondari, zahanati na vituo vya afya. Ujenzi wa mifumo ya maji kazi inaendelea.”

“Umeme wa REA pia utakuwepo. Huku malipo hakuna umeme. Haya tutayafanya na Rais Samia amesisitiza tuyafanye ili wananchi msipate bughudha,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Aliwaeleza viongozi hao wa kimila kwamba Rais Samia ameridhia eneo lao la kufanyia ibada za kimila liendelee kutumika kwa sababu ni jambo jema. “Maeneo yote ya kimila, wananchi waruhusiwe kuendesha mila zao. Mkuu wa Mkoa simamia hili, ilimradi mkuu wa chuo apewe taarifa mapema kwamba mnakuja lini kunafanyika shughuli yenu,”alisema.

Mapema, Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Isack Ole Kisongo, alisema kwa nafasi yao viongozi wa kimila wako tayari kushirikiana na serikali kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote.

“Kwa kunyanyua rungu zetu tumekula kiapo kwa kukubali kuwa Ngorongoro na hifadhi nyingine nchini zilindwe kwa nguvu zote ili hadhi yake irudi kama zamani,” alisema Kisongo.

Alisema suala la kuhama Ngorongoro halina tofauti na maeneo mengine ambako wananchi waliondoka kwa amani kupisha miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa reli ya kisasa, bomba la mafuta la kutoka Tanga hadi Uganda na ukuta wa Mererani.

Naye Laigwanan wa Malaigwanan wa Ngorongoro, Mzee Matengway Ole Tauwo, alimweleza Waziri Mkuu Majaliwa kwamba anasubiri kwa hamu tarehe ya kuhamia huko kwa sababu ameenda hadi Handeni na ameona kwa macho yake kwamba mipango ya serikali ina lengo zuri.

“Nataka uniambie leo tarehe gani mkuu wa mkoa ananipeleka huko, niko tayari kwenda. Mke wangu alipoona ile nyumba alitaka kugoma kurudi tena Ngorongoro. Nataka nijue tarehe ya kwenda sababu hapa sina hatimiliki, siwezi kulima, lakini kule naweza,” alisema mzee huyo mwenye umri wa miaka 70.

Akisoma risala kwa niaba ya Malaigwanan hao, Katibu Mkuu wa Jamii hiyo, Amani Lukumay alisema wanayo maeneo ya kimila ambayo yametishiwa kuchukuliwa na akaomba serikali iingilie kati ili maeneo hayo yakabidhiwe rasmi kwao.

NA MWANDISHI WETU

Abdurahman Jumanne

Abdurahman Jumanne

Stay Connected test

  • 111 Follower
  • 168k Subscriber
  • 23.5k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
MBUNGE LINDI ATAKA VIJANA WAJISHUGHULISHE

MBUNGE LINDI ATAKA VIJANA WAJISHUGHULISHE

July 8, 2021
JAFO AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA MARA KUJIKITA KATIKA ZAO LA ALIZETI

JAFO AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA MARA KUJIKITA KATIKA ZAO LA ALIZETI

0
KIHONGOSI : NGORONGORO MCHAGUENI SHANGAI

KIHONGOSI : NGORONGORO MCHAGUENI SHANGAI

0
JWTZ IKO IMARA KUKABILI MATUKIO YA KIGAIDI-SERIKALI

JWTZ IKO IMARA KUKABILI MATUKIO YA KIGAIDI-SERIKALI

0
MAJALIWA AANIKA SIRI UJENZI VYUO VYA VETA

MAJALIWA AANIKA SIRI UJENZI VYUO VYA VETA

0
MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

May 20, 2022
SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

May 20, 2022
RAIS SAMIA: MAWAZIRI CHAPENI KAZI, MSISIKILIZE MANENO

RAIS SAMIA: MAWAZIRI CHAPENI KAZI, MSISIKILIZE MANENO

May 20, 2022
TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

May 18, 2022

Recent News

MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

May 20, 2022
SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

May 20, 2022
RAIS SAMIA: MAWAZIRI CHAPENI KAZI, MSISIKILIZE MANENO

RAIS SAMIA: MAWAZIRI CHAPENI KAZI, MSISIKILIZE MANENO

May 20, 2022
TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

May 18, 2022
Instagram Youtube Twitter VK Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • 2021
  • Afya Makala
  • BURUDANI
  • Business
  • GAZETI LA BURUDANI
  • GAZETI LA UHURU
  • GAZETI LA UHURU MACHI 17
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • KIMATAIFA
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • RIWAYA
  • SIASA
  • Uncategorized

Recent News

MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

May 20, 2022
SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

May 20, 2022

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In