ALIYEKUWA Mbunge wa Shinyanga Mjini na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Afrika (PAP), Stephen Masele, amechukua fomu ya kuwania Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika ofisi Ndogo za CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Masele amesema “ Ni matakwa ya Katiba, Mtanzania yeyote mwenye sifa anaweza kugombea nafasi ya Uspika, nimetumia nafasi yangu kama Mtanzania Mwanachama hai wa CCM, kuomba ridhaa ya Chama changu kunifikiria katika nafasi hii ya Uspika.”
Uwezo Ninao, Uzoefu Ninao, ninaimani nikifanikiwa kuwa Spika nitaweza kusimamia Shughuli za Serikali.” Amesema Stephen Masele