POLISI Mkoa wa Pwani, imemkamata mtuhumiwa aliyekuwa akitafutwa kwa matukio ya uvunjaji na uporaji wa pikipiki.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani, ACP Wankyo Nyigesa, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa Rashid Shabani (24), mkazi wa Mtaa wa Saidi Domo.
Amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Desemba 28, mwaka huu, saa 12:30 jioni, Mlandizi A mtaa wa Said Domo, tarafa ya Mlandizi.
Kamanda Wankyo amesema mtuhumiwa huyo baada ya kupekuliwa alikutwa na pikipiki na vifaa vya kuvunjia.
Pia, alikutwa na simu mbili za mkononi na waleti na vitambulisho vyenye majina ya Edward Joseph Chewale.
Amesema mtuhumiwa huyo katika mahojiano, aliwataja wenzake watatu aliokuwa akishirikiana nao katika matukio hayo ya uvunjaji na uporaji wa pikipiki ambao walikamatwa na majina yao yamehifadhiwa.
Amesema wanaendelea na msako wa watu wengine watano wanaotumia gari kwenda mji wa Kibaha kufanya matukio ya utapeli wa fedha.
Na Scolastica Msewa, Kibaha