WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imekabidhi vifaa vya kujikinga na Uviko- 19 kwa mikoa 12 ya Tanzania Bara na mitano ya Zanzibar.
Vifaa hivyo vimetolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kupitia Shirika la Kimataifa la Nutrition International (NI) ikiwa ni kuwakinga watoa huduma ya afya hususani katika utoaji wa matone ya vitamini A nchini.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa wawakilishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mganga Mkuu wa Serikali, Aifi llo Sichalwe, alisema vifaa hivyo vitakwenda kuwasaidia watoa huduma za afya walio mstari wa mbele katika kutoa huduma za afya nchini, bila kuwasahau watoa huduma za afya ngazi ya jamii (CHW).
Vifaa vilivyotolewa ni katoni 6,000 za barakoa na vitakasa mikono 6,000 vyenye gharama ya sh. milioni 57 vimetolewa na vitasambazwa katika mikoa 17.
Dk. Sichalwe alisema kutokana na changamoto ya Uviko -19, serikali inaendelea kuwapatia vifaa vya kujikinga na maambukizi hayo watoa huduma waliopo katika vituo vya afya ili kuwawezesha kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi ikiwemo kampeni ya utoaji wa matone ya vitamini A inayofahimika kama huduma ya mwezi wa afya na lishe ya mtoto.
“Vifaa hivi vimeanza kutolewa katika mikoa 12 ya Dodoma, Geita, Kagera, Morogoro, Katavi, Mwanza, Kilimanjaro, Shinyanga, Simiyu, Singida, Tabora, Tanga na mikoa mitano ya Tanzania Visiwani.
“Mikoa hii imeteuliwa kwa sababu ilikuwa na ufanisi duni katika utoaji wa huduma za mwezi wa afya, hivyo kupitia msaada huu utasaidia kuimarisha kiwango cha katika utoaji wa huduma za matone ya vitamini A kwa watoto wengi zaidi,” alisema.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dk. Ray Masumo, aliishukuru Serikali ya Canada kupitia NI kwa kuendelea kuiunga mkono serikali katika vita dhidi ya Uviko-19 na changamoto nyingine za kilishe.
Dk. Masumo alisema vifaa hivyo vitawasaidia watoa huduma ya afya waliopo mstari wa mbele katika kutoa huduma za afya ikiwemo huduma ya mwezi wa afya na lishe ya mtoto, kwani malengo yaliyopo ni kuhakikisha ifi kapo mwaka 2025 watoto wote nchini wafi kiwe na huduma ya matone hayo kupitia vituo vya afya vilivyopo nchini.
Naye, Mkurugenzi Mkazi wa NI, Dk. Daniel Nyagawa, alisema wamechukua uamuzi wa kutoa vifaa kwa serikali ikiwa kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazochukuliwa katika kupambana na Uviko -19 na wataendelea kushirikiana katika afua nyingine ikiwemo zile za kilishe ambazo shirika hilo limekuwa likizitekeleza nchini.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Ofi si ya Rais-TAMISEMI, Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Dk.Mwanahamisi Hassan, alisema vitawasaidia watoa huduma za afya waliopo mstari mbele katika vita ya Uviko-19, hivyo anawakaribisha wadau wengine kujitokeza katika kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na serikali katika vita hiyo.
Na Mwandishi Wetu