MKANDARASI wa Ujenzi wa kulinda Kingo za Bahari katika Ufukwe wa Coco, amepatikana, na ujenzi utaanza wakati wowote kwa Mawe kupangwa ili kuzuia mmomonyo wa Kingo za Bahari.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwalinda Wafanyabiashara kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla, leo amekabidhi kazi ya ujenzi wa Kingo za Kuzuia Maji ya Bahari kwenda kwenye Vibanda vya Machinga eneo la Coco Beach.
Mkandarasi huyo ataanza kazi ya kupanga Mawe na kujenga Garden ya Kisasa ya Vigae katika eneo la mbele ya Vibanda ambalo kwa sasa limetawaliwa na Vumbi.
Serikali imedhamiria kufanya Ufukwe wa Coco kuwa kimbilio la wananchi kwa ajili ya Matembezi, Mapumziko, Chakula na Vinywaji.