Monday, May 16, 2022
27 °c
Dar es Salaam
25 ° Thu
25 ° Fri
25 ° Sat
25 ° Sun
25 ° Mon
English EN Kiswahili SW
UHURU MEDIA GROUP
Tangaza Nasi
  • Mwanzo
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

    NI HISTORIA NYINGINE CCM

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM ITAENDELEA KUWA CHAMA BORA, IMARA AFRIKA- SHAKA

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
  • Michezo
    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    PABLO AIPANIA KMC 

    PABLO AIPANIA KMC 

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • UMG
    • Home
    • About Us
    • Services
    • Shop
    • Contact Us
  • MAGAZETI
    • Uhuru wanawake
    • Mzalendo
    • Uhuru vijijini
    • Burudani
    • Uhuru kijani
  • UHURU FM
    • Ratiba
  • UHURU DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • Mwanzo
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

    NI HISTORIA NYINGINE CCM

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM ITAENDELEA KUWA CHAMA BORA, IMARA AFRIKA- SHAKA

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
  • Michezo
    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    PABLO AIPANIA KMC 

    PABLO AIPANIA KMC 

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
No Result
View All Result
UHURU MEDIA GROUP
No Result
View All Result
Mwanzo Habari Kitaifa

MNDEME AGUSWA NA UTOAJI MIKOPO BILA RIBA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 16, 2021
in Habari Kitaifa
0 0
0
MNDEME AGUSWA NA UTOAJI MIKOPO BILA RIBA

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Christine Mndeme

0
SHARES
53
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Christine Mndeme, amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ndiyo pekee yenye kutoa mikopo kwa wajasiriamali pasipo kutoza riba tofauti na serikali zingine duniani.

Pia, amewataka vijana, kinamama na wenye ulemavu kuchangamkia fursa hiyo kwa sababu fedha zipo na zinatolewa kwa waliokidhi vigezo.

Kauli hiyo aliitoa wilayani humo wakati akizungumza na wajasiriamali wanufaika wa fedha za mikopo ya asilimia 10 iliyotolewa na Halmashauri ya Missenyi, Mkoa wa Kagera.

“Tunasema pochi la mama limefunguka, fedha zipo zichangamkieni. Ni serikali gani ambayo inatoa mikopo bila riba duniani?. Ni serikali ya Rais Samia pekee ndio inatoa mikopo bila riba kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wake,” alieleza huku akishangiliwa na wanufaika wa mikopo hiyo.

Alizitaka halmashauri kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu ambao wana ujuzi wa kushiriki miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule na afya inayotekelezwa na serikali.

“Ipo miradi ya ujenzi wa madawati, madirisha kwenye shule. Kama kuna wenye ulemavu wana uwezo wa kuitekeleza wapewe na hii itasaidia zaidi kuwainua kiuchumi,” alieleza.

Alisema Ilani ya uchaguzi ya CCM imeeleza itatoa ajira rasmi na zisizokuwa rasmi kwa makundi yote na ndio sababu ya kuanza kutoa mikopo kwa wajasiriamali kupitia halmashauri.

Mndeme alieleza kwamba wanufaika wa mikopo hiyo ni muhimu wakatumia kwa malengo waliyokusudia pamoja na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.

Aliziagiza halmashauri kuendelea kutoa mikopo na elimu kwa wajasiriamali kuchangamikia fursa za masoko yaliyopo hususan katika maeneo ya mipakani.

Alisema Wilaya ya Missenyi ina fursa nyingi za kibiashara zinazoweza kufanyika katika eneo la mpaka wa Tanzania na Uganda ikiwemo vijana wa bodaboda kubeba abiria.

Hata hivyo, aliwataka vijana wa bodaboda kuacha kufanya biashara za magendo mipakani na kusafirisha wahamiaji haramu kwani ni kinyume cha sheria za nchi.

Kwa upande wake, mjasiriamali mwenye ulemavu wa viungo, Selestine Mukandara, alitoa salamu za shukrani kwa Rais Samia kwani wenye ulemavu wamekuwa sehemu ya wanufaika kupitia mikopo hiyo.

Mukandara ambaye anajishughulisha na ufundi wa kuchomelea na kutengeneza majiko, alisema amechukua mikopo awamu tatu kupitia halmashauri ya Missenyi iliyomwezesha kupanua wigo wa biashara yake.

“Safari hii nimechukua sh. milioni mbili ambazo natarajia kuongeza mtaji wa shughuli zangu. Nimeweza kutengeneza milango, pikipiki ya wenye ulemavu na majiko. Lakini pia nimeaandaa andiko la kuanzisha kampuni yangu,” alieleza.

Naye, Mwenyekiti wa Kikundi cha Uaminifu Omukitwe kinachojishughulisha na biashara ya bodaboda, Johannes Patrick, alisema kikundi hicho cha vijana kimepatiwa mikopo wa sh. milioni 15.

Alisema fedha hizo zimetumika kununulia pikipiki ambazo kila mwanachama anazitumia kwa shughuli za kubeba abiria.

“Tunaomba umfikishie salama mama yetu Rais Samia, kwamba fedha zipo na tunazipata. Hapa tunakopa kwa thamani ya bei ya pikipiki sokoni na tunarudisha mkopo bila riba.

Alibainisha kuwa: “Mafanikio ni makubwa kwa sababu mkopo huu ni nafuu kwani marejesho yake sawa na sh. 7,000 kwa siku hadi utakapokamilisha tofauti na pikipiki za watu binafsi, ambapo tunatakiwa kutoa hesabu kwa mmiliki sh. 10,000 kwa siku kwa kipindi cha miezi 12 hadi 13.”

Hata hivyo, aliiomba serikali kutatua changamoto ya kutozwa sh. 17,000 kwa mwaka na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) , wakati bado pikipiki hizo zinahesabika kama mali ya halmashauri  kwa sababu bado hawajakamilisha kurejesha mkopo.

Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi katika kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu, imetoa mikopo ya sh. milioni 302 kwa vikundi 36 vya wakina mama, vijana na wenye ulemavu.

Fedha hizo ni sehemu ya utekelezaji wa takwa la kisheria linalozitaka halmashauri nchini kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kutoa mikopo kwa makundi hayo ya wajasiriamali.

NA MUSSA YUSUPH, MISSENYI

Abdurahman Jumanne

Abdurahman Jumanne

Stay Connected test

  • 110 Follower
  • 168k Subscriber
  • 23.5k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
MBUNGE LINDI ATAKA VIJANA WAJISHUGHULISHE

MBUNGE LINDI ATAKA VIJANA WAJISHUGHULISHE

July 8, 2021
SHAKA AWAHIMIZA WATANZANIA KUCHAPAKAZI KUINUA UCHUMI

SHAKA AWAHIMIZA WATANZANIA KUCHAPAKAZI KUINUA UCHUMI

0
TTCL YAJIVUNIA UTOAJI HUDUMA WA MAWASILIANO KIMATAIFA

TTCL YAJIVUNIA UTOAJI HUDUMA WA MAWASILIANO KIMATAIFA

0
KIKONGWE KUHITIMU PHD

KIKONGWE KUHITIMU PHD

0
MKUTANO WA KIHISTORIA KATIKA HISTORIA YA MIAKA 100 YA CPC

MKUTANO WA KIHISTORIA KATIKA HISTORIA YA MIAKA 100 YA CPC

0
UWT TEMEKE KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

UWT TEMEKE KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

May 11, 2022
DK. MWINYI ASEMA HAKI KICHOCHEO CHA AMANI NCHNI

DK. MWINYI ASEMA HAKI KICHOCHEO CHA AMANI NCHNI

May 11, 2022
SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

May 11, 2022
MABEHEWA MAPYA 22 KUNUNULIWA

MABEHEWA MAPYA 22 KUNUNULIWA

May 11, 2022

Recent News

UWT TEMEKE KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

UWT TEMEKE KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

May 11, 2022
DK. MWINYI ASEMA HAKI KICHOCHEO CHA AMANI NCHNI

DK. MWINYI ASEMA HAKI KICHOCHEO CHA AMANI NCHNI

May 11, 2022
SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

May 11, 2022
MABEHEWA MAPYA 22 KUNUNULIWA

MABEHEWA MAPYA 22 KUNUNULIWA

May 11, 2022
Instagram Youtube Twitter VK Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • 2021
  • Afya Makala
  • BURUDANI
  • Business
  • GAZETI LA BURUDANI
  • GAZETI LA UHURU
  • GAZETI LA UHURU MACHI 17
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • KIMATAIFA
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • RIWAYA
  • SIASA
  • Uncategorized

Recent News

UWT TEMEKE KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

UWT TEMEKE KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

May 11, 2022
DK. MWINYI ASEMA HAKI KICHOCHEO CHA AMANI NCHNI

DK. MWINYI ASEMA HAKI KICHOCHEO CHA AMANI NCHNI

May 11, 2022

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In