WIZARA ya Mawasiliano na Teknologia ya Habari imesaini mkataba na Shilika la Nyumba (NHC), wa kiasi cha Shilingi bilioni 23,948 kwaajili ya kuanza kwa ujenzi wa jengo la wizara hiyo litakalo jengwa katika eneo la mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo Waziri wa Habari na Teknologia ya Mawasiliano, Dk.Ashatu Kijaji, amesema serikali imetenga fedha hizo kwaajili ya kukamilishwa kwa haraka mradi huo wa ujenzi wa ofisi za wizara hiyo ambayo ni mpya ili ianze kusimamia shughuli zake.
Aidha, amewataka wakandalasi waliopewa kusimamia mradio huo ambao ni Shirika Nyumba (NHC) kuweza kufanya kazi kizarendo na kiufanisi kwa ubora wa hali ya juu ili kukidhi viwango bora vya majengo ya serikali.
“Leo tumekutana hapa kwa lengo la kuhakikisha tunafanya makubaliano kuanza kwa ujenzi wa Wizara yetu na nacho waomba sana wasimamizi wa mradi huu kufanya kwa haraka kwa ustadi mzur na wakisasa.

“Tunaishukuru sana serikali kwa kutuona sisi na kutupatia nafasi ya kwanza kwa ujenzi wa awamu ya pili wa majengo ya mji wa kiserikali pia naimani kubwa na ubia tulioingia na NHC kulingana na kazi zao tunaziona hivyo hatuna shaka mradi huu utaenda kiustadi”.amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba Taifa, Dk. Maulid Banyani, amesema watajitahidi kukamilisha mradi huko kwa muda muafaka na ubora wa kitaalam kwani kwa muda mrefu serikali imekuwa ikiwaamini kwa kuwapatia fursa za miradi mbalimbali na kwa kushirikiana na Wakala wa majengo ya serikali katika kusimamia mradii huo unakuwa wa viwango stahiki.
“Sisi kama Shirika la NHC tunaahidi kusimamia mradi huu uende kulingana na bajeti tuliyokubaliana na wizara na kwa kuingua ubia huu sasa kazi hii itaanza haraka iwezekanavyo na kukamilika kwa muda maalumu”. Alisema Dk. Banyani.
Na Benedict Mwasapi