SERIKALI imesema Itawachukulia hatua kali ikiwemo kulipa au kujenga upya miradi ya barabara itakayokamilika kisha kubainika imejengwa chini ya viwango stahiki.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, wakati alipotembelea eneo la Mradi wa Barabara ya Tanga-Pangani mkoani Tanga.
Amesema kumekuwa na tatizo hilo hali inayopelekea miradi ya barabara kuigharimu serikali fedha nyingi huku zikijengwa chini ya viwango.
Aidha, amebainisha kuwa hali hiyo hupelekea serikali kuingia upya gharama za matengezo ya mara kwa mara.
“Serikali imenunua gari maalumu ambayo ina vifaa vya kupima ubora wa barabara hivyo tukibaini ipo barabara imejengwa chini ya kiwango basi mkandarasi atawajibika kulipa kwa kujenga upya barabara hiyo,” amesema Waziri Mbarawa.
Na Susan Uhinga, Tanga