RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameelekeza kupunguzwa kwa tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali katika bidhaa za mafuta hapa nchini zenye thamani ya Shilingi Bilioni 102 kwa mwaka, kwa lengo la kupunguza bei za mafuta ili kuwapa unafuu wananchi.
Rais Samia amechukua hatua hiyo ili kukabaliana na upandaji wa bei za mafuta katika soko la dunia ambapo kwa muda mrefu imekuwa ikipanda kwa kiwango kikubwa na kuathiri watumiaji wa bidhaa hiyo hapa nchini.