MKUU wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila, ametoa siku tano kuanzia leo, wakulima wote wa zao la pamba mkoani humo ambao bado hawajaondoa masalia ya pamba katika mashamba yao, kuhakikisha wanaondoa mara moja kabla ya siku ya Okt 15, 2021.
Amesema kuondoa masalia kwenye shamba kwa mkulima wa zao la pamba ni sheria wala siyo hiari, ambapo ameleza hadi kufikia siku hiyo kila mkulima wa zao hilo anatakiwa kuwa ameteleleza agizo hilo la kisheria.
“sheria inawataka wakulima wa pamba kila mwaka ifikapo Sept 15, 2021 muwe mmeondoa masalia na magugu yote kwenye mashamba yanu na mkulima atakayekaidi anatakiwa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria hiyo… sheria inaelekeza kila mkulima kuondoa masalia pamoja na magugu kwenye shamba lake, na ambaye atakaidi atatakiwa kutozwa faini ya shilingi elfu 50,000 au kifungo cha miezi sita jela au vyote kwa pamoja”amesema RC Kafulila
Aidha, amesema mkoa huo umejidhatiti kuhakikisha unazalisha tani laki tano za pamba katika msimu huu huku akiwataka watendaji wa kata kuhakikisha baada ya muda uliotolewa kuisha, watekeleza kwa vitendo sheria hiyo kwa mtu yeyote ambaye atakaidi kutii.
Na Anita Balingilaki, Meatu.