SERIKALI ya Awamu ya Sita inagusa maisha ya kila Mtanzania kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ambao unaziwezesha kaya maskini nchini kupata ruzuku inayozisaidia kuboresha maisha yao.
Hali hiyo imesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chenene na Kwahemu, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ndejembi, amesisitiza kuwa katika kuhakikisha fedha za mradi zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali inawaasa wanufaika wa TASAF kutumia ruzuku wanayoipata kuboresha maisha yao badala ya kufanya Anasa.

Pia amewataka Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuweka mkakati wa kuboresha maisha yao kupitia TASAF, kwani haoni sababu ya wanaonufaika kutumia fedha hizo tofauti na malengo yaliyokusudiwa na Serikali.
Na MWANDISHI WETU