SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa kiasi Cha Sh 1.499 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wasichana katika Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC) lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 420 ili kukidhi mahitaji ya hosteli kwa wasichana wanaojiunga na chuo hicho.
Uongozi wa ATC unaeleza kuwa awali kulikuwa na muamko mdogo wa wasichana kujiunga na chuo hicho lakini hivi sasa kunaongezeko la wasichana ambapo wanafikia 4000 kutoka 400 waliokuwepo mwaka 2000.
Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dk. Yusuph Mhando ameeleza hayo wakati wa ziara maalum ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali iliyoandaliwa na wizaya hiyo kwa ajili ya kutembelea miradi mbalimbali na kuangalia utekelezaji wake kutokana na fedha zinazotolewa na serikali.
“Tulikuwa na idadi ndogo ya wanafunzi wasicha, tulipoanza kuwapata changamoto ikawa ni mahali pakulala, tunaishukuru serikali ilitupatia fedha kama ruzuku kutoka serikalini tumejenga mabweni ya hosteli ya wasichana ikiwa ni jitihada za kukabiliana na hiyo ya upungufu wa mabweni,”amesema.
Dk. Mhando amesema kuwa fedha hizo zitatumika kujenga mabweni ya wasichana ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 420.
“Wanafunzi wa kike wamehamasika kusoma masomo ya sayansi hivyo kunauhitaji wa mabweni katika chuo,” amesema Dk.Mhando.
Kaimu mkuu wa chuo hicho amebainisha kuwa, mpaka sasa ujenzi huo unaotekelezwa na wakandarasi wa ndani (force account) umefikia asilimia 15.
Pia amesema chuo kimepokea sh. Milioni 765 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya majisafi na majitaka, ununuzi wa samani na majengo.
Akizungumzia fedha hizo Sh 765 milioni, amesema fedha hizo zimetumika katika ukarabati wa miundombinu ya majisafi na majitaka, majengo na ununuzi wa samani, zimetumika katika ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji.
Dk. Mhando amesema awali walikuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita 145,000 jambo ambalo lilikuwa halitoshelezi mahitaji ya chuo hicho lakini baada ya ujenzi huo hivi sasa wanaweza kuhifadhi lita milioni 1.2.
Amesema katika kuwezesha kuwapatia wanafunzi na watumishi huduma za afya na kwa haraka chuo kilianza ujenzi wa kliniki kwa kutumia mapato yake ya ndani.
“Mradi Mradi ulianza mwishoni mwa mwezi Mei, 2021 ambapo utekelezaji umefikia Asilimia 15 na upo katika hatua za ujenzi wa msingi (substructure) Mradi unatekelezwa kwa njia ya Force A,”amesema.
Kwa upande wake, Msajili wa wanafunzi wa chuo hicho, Dk.Baraka Kichonge amesema kuwa idadi hiyo ya wanafunzi wa kike imeongeka kutoka 400 mwaka 2,000 hadi kufikia 4,000 mwaka huu.
Na Happiness Mtweve, Arusha