Saturday, May 21, 2022
27 °c
Dar es Salaam
25 ° Thu
25 ° Fri
25 ° Sat
25 ° Sun
25 ° Mon
English EN Kiswahili SW
UHURU MEDIA GROUP
Tangaza Nasi
  • Mwanzo
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

    NI HISTORIA NYINGINE CCM

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM ITAENDELEA KUWA CHAMA BORA, IMARA AFRIKA- SHAKA

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
  • Michezo
    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    PABLO AIPANIA KMC 

    PABLO AIPANIA KMC 

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • UMG
    • Home
    • About Us
    • Services
    • Shop
    • Contact Us
  • MAGAZETI
    • Uhuru wanawake
    • Mzalendo
    • Uhuru vijijini
    • Burudani
    • Uhuru kijani
  • UHURU FM
    • Ratiba
  • UHURU DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • Mwanzo
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

    NI HISTORIA NYINGINE CCM

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM ITAENDELEA KUWA CHAMA BORA, IMARA AFRIKA- SHAKA

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
  • Michezo
    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    PABLO AIPANIA KMC 

    PABLO AIPANIA KMC 

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
No Result
View All Result
UHURU MEDIA GROUP
No Result
View All Result
Mwanzo Habari Kitaifa

SHAKA ATOA MWEZI MMOJA MAJI YAFIKE KWA WANANCHI

186>>> Kifungu cha Ilani CCM kinachoonyesha Rais Mwinyi atakavyopeleka maji kwa wananchi

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 29, 2022
in Habari Kitaifa
0 0
0
CCM YATIA MKONO TRILIONI 1.3/- ZA IMF

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka

0
SHARES
45
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, ametoa mwezi mmoja kwa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), kuhakikisha wananchi wanapata majisafi na salama kupitia mradi wa tanki la Kikwajuni ambalo limekamilika, lakini halijaanza kutoa huduma.

Ameonya kutofanya kazi kwa ufanisi miradi iliyotumia fedha za wananchi kutekelezwa ikiwamo kufanyika kwa upembuzi yakinifu kabla ya kuanza kwa utekelezaji, ni kumhujumu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindu, Dk. Hussein Ali Mwinyi na kuichonganisha serikali na wananchi, jambo ambalo Chama hakitaruhusu litokee.

Shaka aliyasema hayo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 katika jimbo la Kikwajuni Mkoa wa Mjini Unguja, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, Visiwani Zanzibar.

“Kifungu cha 186 cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, kinaonyesha jinsi Rais Mwinyi atakavyopeleka maji kwa wananchi.

“Kwa namna yoyote, kutotimia kwa miradi ya maendeleo ni kumhujumu Rais. Nakupeni mwezi mmoja, maji yatoke hapa,” aliagiza Shaka kwa ukali baada ya kutoridhishwa na maelezo ya wataalamu wanaosimamia mradi huo.

Alieleza kuwa, CCM inazo taarifa za ziada juu ya kutofanya kazi kwa mradi huo uliotarajiwa kuleta ahueni kubwa ya huduma ya maji safi kwa wananchi, huku akisema taarifa hizo, zinaonyesha kuna mikono ya baadhi ya watu wasiotaka ufanye kazi kwa maslahi yao.

Shaka alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya Awamu ya Nane, chini ya Rais Dk. Mwinyi, inafanya kazi kubwa kuleta maendeleo, hivyo CCM haitakubali kuona jitihada hizo zikiwekewa vizingiti na baadhi ya watu na hatimaye zishindwe kuleta nafuu ya maisha kwa wananchi.

“Kumkwamisha Rais Mwinyi ni kuwakwamisha wananchi. Haiwezekani mradi huu, tangu mwaka 2018 hadi leo usitoe maji. Viongozi wakubwa wamekuja katika mradi huu, CCM haitakubali kuona ukiendelea kutotoa huduma, wahusika jipangeni ndani ya mwezi mmoja maji yatoke hapa, nasi tutaufuatilia kwa karibu kuona maagizo haya yanafanyiwa kazi kwa kiasi gani,” alisema.

Kauli ya Shaka ilikuja baada ya Mbunge wa Kikwajuni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuph Masauni, kukiomba Chama kisaidie kusukuma mradi huo ili utoe maji baada ya juhudi zao kugonga mwamba kwa muda mrefu.

Masauni alisema kuwa, mradi huo umetekelezwa na fedha nyingi ambazo yeye binafsi na viongozi wenzake, walihangaika kuzitafuta kwa wafadhili, lakini licha ya tanki kujengwa na miundombinu mingine kukamilika haujaanza kutoa maji kama ilivyotarajiwa.

Akitoa maelezo kuhusu mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa ZAWA, Dk. Salha Mohamed Kassim, alikiri mradi kutoafanya kazi kwa muda mrefu, ingawa umekamilika na kwamba, hilo linatokana na chanzo kilichotarajiwa kujaza maji katika tanki hilo kutokuwa na uwezo kwa sasa wa kutosheleza ujazaji maji.

Hata hivyo, alisema kuna mikakati ya dharura ya kuhakikisha tanki hilo linajazwa maji kwa ajili ya kupeleka huduma kwa wananchi wakati jitihada za kupata maji ya kutosha kulijaza kama ilivyokusudiwa zikiendelea kufanyika.

Katika ziara hiyo, Shaka pia alitembelea Kituo cha Afya Rahaleo ambako alikagua maboresho mbalimbali yaliyofanywa na serikali katika huduma za afya kituoni hapo ukiwemo ukarabati wa majengo na kufunga vifaa vya kisasa kisha kuzungumza na watumishi wa kituo hicho.

Alitembelea na kushiriki kikao katika Shina Namba 4, Tawi la CCM Kikwajuni Juu ambako aliwakumbusha vijana nafasi yao katika ulinzi wa Chama na kushiriki shughuli za maendeleo, huku akisema Chama kinatambua kilio chao kuhusu ajira.

Na MWANDISHI WETU, Zanzibar

Abdurahman Jumanne

Abdurahman Jumanne

Stay Connected test

  • 111 Follower
  • 168k Subscriber
  • 23.5k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
MBUNGE LINDI ATAKA VIJANA WAJISHUGHULISHE

MBUNGE LINDI ATAKA VIJANA WAJISHUGHULISHE

July 8, 2021
JAFO AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA MARA KUJIKITA KATIKA ZAO LA ALIZETI

JAFO AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA MARA KUJIKITA KATIKA ZAO LA ALIZETI

0
KIHONGOSI : NGORONGORO MCHAGUENI SHANGAI

KIHONGOSI : NGORONGORO MCHAGUENI SHANGAI

0
JWTZ IKO IMARA KUKABILI MATUKIO YA KIGAIDI-SERIKALI

JWTZ IKO IMARA KUKABILI MATUKIO YA KIGAIDI-SERIKALI

0
MAJALIWA AANIKA SIRI UJENZI VYUO VYA VETA

MAJALIWA AANIKA SIRI UJENZI VYUO VYA VETA

0
MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

May 20, 2022
SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

May 20, 2022
RAIS SAMIA: MAWAZIRI CHAPENI KAZI, MSISIKILIZE MANENO

RAIS SAMIA: MAWAZIRI CHAPENI KAZI, MSISIKILIZE MANENO

May 20, 2022
TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

May 18, 2022

Recent News

MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

May 20, 2022
SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

May 20, 2022
RAIS SAMIA: MAWAZIRI CHAPENI KAZI, MSISIKILIZE MANENO

RAIS SAMIA: MAWAZIRI CHAPENI KAZI, MSISIKILIZE MANENO

May 20, 2022
TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

May 18, 2022
Instagram Youtube Twitter VK Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • 2021
  • Afya Makala
  • BURUDANI
  • Business
  • GAZETI LA BURUDANI
  • GAZETI LA UHURU
  • GAZETI LA UHURU MACHI 17
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • KIMATAIFA
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • RIWAYA
  • SIASA
  • Uncategorized

Recent News

MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

MIPAKA YA TANZANIA IPO SHWARI

May 20, 2022
SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

SERIKALI YATOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU

May 20, 2022

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In