Friday, May 20, 2022
27 °c
Dar es Salaam
25 ° Thu
25 ° Fri
25 ° Sat
25 ° Sun
25 ° Mon
English EN Kiswahili SW
UHURU MEDIA GROUP
Tangaza Nasi
  • Mwanzo
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

    NI HISTORIA NYINGINE CCM

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM ITAENDELEA KUWA CHAMA BORA, IMARA AFRIKA- SHAKA

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
  • Michezo
    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    PABLO AIPANIA KMC 

    PABLO AIPANIA KMC 

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • UMG
    • Home
    • About Us
    • Services
    • Shop
    • Contact Us
  • MAGAZETI
    • Uhuru wanawake
    • Mzalendo
    • Uhuru vijijini
    • Burudani
    • Uhuru kijani
  • UHURU FM
    • Ratiba
  • UHURU DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • Mwanzo
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

    NI HISTORIA NYINGINE CCM

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM YATEUA MAKATIBU WA MIKOA NA WILAYA

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAPOKEA TUZO CHAONGOZA KUWA NA WAFUASI WENGI MTANDAONI

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    CHONGOLO APIGILIA MSUMARI FEDHA ZA IMF

    SHAKA ATAJA SIRI CCM KUKUBALIKA

    CCM ITAENDELEA KUWA CHAMA BORA, IMARA AFRIKA- SHAKA

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    MBISE ATOA VITI MIA MOJA MONDULI

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
  • Michezo
    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    SIMBA, KAGERA NI KISASI, HESABU LEO

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    HAPATOSHI BURKINA FASO, SENEGAL  AFCON

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    MAYELE AIPA JEURI YANGA

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    NABI KUTUMIA MASTAA WAPYA MAPINDUZI CUP

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    SIMBA KIMATAIFA HATOKI MTU

    PABLO AIPANIA KMC 

    PABLO AIPANIA KMC 

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
No Result
View All Result
UHURU MEDIA GROUP
No Result
View All Result
Mwanzo RIWAYA

SIKU YANGU YA KWANZA KABURINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 13, 2021
in RIWAYA
0 0
0
SIMULIZI YA SIKU YANGU YA KWANZA KABURINI

SEHEMU YA 4

0
SHARES
194
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

SEHEMU YA 2

MTUNZI: CHRISTOPHER LISSA

ISBN ….978-9987-9886-1-7

(Toa maoni ya simulizi hii 0654 58 67 88, 0629 643 419)

ILIPOISHIA……

Naam! Nilipogeuka  na kutazama upande wa kile kimsitu cha mikorosho ya Mputa,  niliona moto mkubwa ukiwaka juu kabisa ya miti hiyo. Ulikuwa ni moto mkubwa sana.

Hata hivyo nilibaini kwamba moto huo licha ya kuwa mkubwa ulikuwa  hauteketezi miti. Ulikuwa ni moto wa miujiza.

Ama kweli dunia hii inamambo na omba  uyasikie tu kwa jirani  lakini yasikutokee.

 

SASA ENDELEA……

 

NURU  ilitanda  katika eneo lote  tulilokuwepo kiasi kwamba   nilikuwa mahari  peupe kabisa.

Nikabaki nimetumbua macho yangu kwa mshangao  mkuu.  Mara nikaanza kusikia kicheko cha ajaabu kikitokea katika msitu huo wa mikorosho.

“Haa ..Haaa… Haaaaa…. Haaaaa  ,” kicheko chenye sauti mbaya yenye mawimbimawimbi  ilipenya sawia katika mifereji ya masikio yangu na kutikisa ngoma za masikio kisha kupeleka taarifa katika ubongo ulioniletea tafsiri ya haraka  kuwa kilicho kuwa kikitokea  mbele yangu ni tukio la muujiza wa kutisha.

Siyo tukio la kutisha tu, bali muujiza wa  kutisha sana. Nikabaki nimeduwaa kama sanamu lililosimikwa katikati ya mbuga hiyo, huku nikiwa nimekodoa macho , akili yangu ikiwa imeruka kwa uoga.

Naam! Sasa ule moto uliokuwa ukiwaka juu ya mikorosho ukajikusanya na kufanya duara moja kubwa.

Taratibu  nikaanza kuona taswira za kiumbe wa ajabu  ikijiunda katikati ya mduara huo. Baada ya sekunde kadhaa kiumbe huyo wa kutisha akawa amejiumba.

Alikuwa ni mwanamke wa kutisha sana, mwenye kichwa cha fuvu jeusi.

Sura yake  ilikuwa ya bibi kizee. Macho yake   makubwa ya duara yalikuwa  mekundu  sana yenye mboni nyeusi kama za paka.

“Haaa! Haaa.. Haaaa,”aliangua kicheko cha kifedhuri.  Alikuwa na ulimu mrefu  uliokuwa ukiwaka moto mwekundu sana.

Alijifunika mtandio mweupe kuzunguka kichwa chake hadi chini ya kidevu. Sehemu ya chini alivaa nguo pana nyeupe  za  hariri.

Alikuwa ni mrefu  sana  lakini mwenye umbo jembamba la duara. Nguo alizo kuwa amevaa zilikuwa zikipepea  kutokana na upepo  uliokuwa ukivuma.

Hata hivyo kwa chini  alikuwa haonekani vema kutokana na kufifia kwake.

Alipokamilika kujiumba, sasa akaanza kupepea angani  na kutoka katika mduara  wa moto kisha  kuja hadi mahari nilipokuwa nimesimama.

Akasimama karibu yangu umbali wa kama  hatua tano hivi, huku akiwa anaelea angani.

“Jini?,” akili yangu iliuliza.

“Hapana Shetani!” nafsi ikajibu haraka.

Hata hivyo  sikuyatilia  uzito  majibu yote mawili, kwa sababu  akili yangu ilikuwa kama imeganda kabisa. Ilikuwa haifanyi kazi sawasawa kutokana na uoga mkuu kunitawala.

Yule kiumbe akanitazama kwa umakini sana huku akigeuza geuza kichwa chake kama vile ananikaagua.

“Haaa! Haaa Haaaa!,” akaangua kile kicheko chake cha maudhi. Kicheko cha sauti mbaya ambacho kiukweli kila alipokuwa akicheka nilihisi mitetemo ya kuoghofya sana.

“Wewe!” akasema kwa sauti ya mitetemo.

“Unauona.. moto.. ule!?”   sasa akaniuliza kwa sauti  ya kawaida, huku akinionyesha moto wa ajabu  uliokuwa ukiwaka juu mikorosho. Hata hivyo sikumjibu.

“Wewe! Umeuona moto ule?” akaniuliza tena. Awamu hii akaongeza sauti. Lakini sikumjibu. Nikamkazia macho kumtazama usoni.

“Nakuuuliza weweee! Umeona motooooo,?” akaniuliza kwa  sauti  ya ukali huku akinisogezea shingo yake na kufanya tutazamane uso kwa uso. Awamu  hii pia sikumjibu….

“Aaaaaaah! Aaaaaah! Waaaaaah!,” Yule kiumbe akaanza kunizunguka  kwa kasi ya ajabu huku akiwa amefura kwa hasira. Akipiga ukulele wa kutisha mno.

Baada ya kunizunguka  akajitokeza tena mbele yangu na kuninitazama kwa  ghadhabu kuu.

“Aaaaaaaagh….,” akapiga ukulele na kuelea kwa kasi kuelekea katika mduara wa moto. Baada ya kuingia tu katika ule mduara moto ukazimika ghafla.

Giza likawa limetanda katika eneo lote na ule upepo wa ajabu uliokuwa ukivuma ulikoma ghafra. Hali ikarudi kama awali. Hali ya kawaida

***

Katika maisha yangu hili ndiyo lilikuwa tukio la kwanza la ajabu nililoshuhudia. Nilikuwa nikisimuliwa tu lakini sasa nilijionea kwa macho.

Istoshe katika kimsitu hiki cha Mputa sikuwahi  kusikia simulizi za kuwepo kwa miujiza ya kutisha kwani shamba hili nililokuwa ninalima lilikuwa lina limwa tangu enzi za babu yangu Lwitiko Lissa, marehemu baba yangu Christopher Mwakitalu na hatimaye mimi.

Hakukuwahi kutokea miujiza  kama hii. Nilipagawa na kusimama kwa eneo hilo kama dakika tano hivi  akili yangu ikiwa haiko sawa kabisa.

Taratibu fahamu ziliendelea kunirudia. Nikapumua pumzi ndefu na kuishusha taratibu, kisha nikakusanya nguvu na kujiweka sawa.

Hatimaye  fahamu zikawa zimenirudia kwa kiasi  fulani kwa sababu tangu muujiza ule ulipoanza kunitokea ilikuwa kama nimehama kabisa  katika dunia hii.

Baada ya kichwa kukaa sawa kidogo  sikuona  umumhimu  wa kuendelea kulima.

Nikaamua kuanza kuwaswaga  makasa wangu kuelekea nyumbani. Kwakweli akili ilikuwa imeivurugika sana.

Wakati ninatembea kutoka shambani  kuelekea nyumbani nilianza kusikia sauti za watu wakiongea.

Kwa  kuwa  barabara ya vumbi  ya  Kapwili kuelekea Kajunjumele hadi Ziwa Nyasa  ilikuwa haiko mbali  na shambani kwangu niling’amua kuwa watu hao huenda walikuwa wanaenda kulima au wasafari wanaenda bandarini ziwani.

Kadiri nilivyo kuwa nikisogea karibu na barabara ndivyo sauti zile za watu   nilikuwa nikizisikia.

Nilibaini kuwa hawakuwa watu wawili au watatu,bali kundi la watu. Hata hivyo nilipotega masikio ili nijue nini walichokuwa wanazungumza  sikuambulia kitu.

Nikiwa nimebakiza kama hatua 15 hivi kufika barabarani,  niliona kundi hilo la watu likipita barabarani.

Nilipotazama kwa makini niliona watu hao kama wamebeba maiti aliyeviringishwa katika shuka jeupe kama siyo sanda.

Maiti huyo ndiyo  alikuwa akionekana  zaidi  kutokana na nguo hizo nyeupe zilizomfanya  kung’ara gizani.

Ng’ombe wakasima. Nywele zikaanza kunisimka tena. Nilihisi kitu kibaya tena kikienda kutokea mbele yangu.

Nikajibanza nyuma ya ng’ombe na kuchungulia vizuri na kwa umakini mkubwa.

Ingawa kulikuwa  giza lakini niliona kama vivuri vya watu. Wakubwa kwa wadogo. Wanawake kwa waume.

Vicheko, vigeregere na sauti za ajabuajabu zilitawala. Lugha waliyokuwa wakiitumia sikuilewa. Pia japo walikuwa wakitembea lakini walikuwa kama wanaelea hewani.

“Wachawi,” hisia zangu zikaniletea jibu.

“Wafu!” akili na hisia vikaanza kubishana tena.

“Majini?,” ubongo ukauliza swali.

“Au mashetani?”  sasa vyote  yaani, akili, hisia, ubongo  vikauliza swali kwa jumla. Hivyo  nikaona vyote havina msaada wa kunipa jibu sahihi. Nikavipuuzia.

Nikaachana navyo nikaona nivema kuhamia moyoni. Huenda moyo ukanipa msaada kwa wakati huo.

Moyo ukanipa ujasiri. Naam! Sasa nikapata mtetezi wangu haswaa. Ujasiri, kwani tukio hili la pili pia  nilikwisha baini ni la kutisha kama lile la mwanzo.

“Hili tena?” nikajiuliuza… USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA 3 YA RIWAYA HII YA KUSISIMUA KESHO

Abdurahman Jumanne

Abdurahman Jumanne

Stay Connected test

  • 111 Follower
  • 168k Subscriber
  • 23.5k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
MBUNGE LINDI ATAKA VIJANA WAJISHUGHULISHE

MBUNGE LINDI ATAKA VIJANA WAJISHUGHULISHE

July 8, 2021
DK. MWINYI ASISITIZA UIMARA WA UCHUMI

DK. MWINYI ASISITIZA UIMARA WA UCHUMI

0
MAJALIWA AANIKA SIRI UJENZI VYUO VYA VETA

MAJALIWA AANIKA SIRI UJENZI VYUO VYA VETA

0
RAIS MUSEVENI AKAMILISHA ZIARA YAKE NCHINI

RAIS MUSEVENI AKAMILISHA ZIARA YAKE NCHINI

0
USWISI KUENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO TANZANIA

USWISI KUENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO TANZANIA

0
TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

May 18, 2022
VIKUNDI VILIVYOPATA MIKOPO YA BILIONI 4/- VYAITWA TAKUKURU

VIKUNDI VILIVYOPATA MIKOPO YA BILIONI 4/- VYAITWA TAKUKURU

May 18, 2022
SHAKA AZIAGIZA WIZARA TATU MISITU YA HIFADHI

SHAKA AZITAKA TAASISI ZA UMMA NCHINI KUTENGA BAJETI ZA MIRADI

May 18, 2022
WIZARA YAANIKA MKAKATI MPYA KUKABILI BEI YA MBOLEA, MAFUTA

WIZARA YAANIKA MKAKATI MPYA KUKABILI BEI YA MBOLEA, MAFUTA

May 18, 2022

Recent News

TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

May 18, 2022
VIKUNDI VILIVYOPATA MIKOPO YA BILIONI 4/- VYAITWA TAKUKURU

VIKUNDI VILIVYOPATA MIKOPO YA BILIONI 4/- VYAITWA TAKUKURU

May 18, 2022
SHAKA AZIAGIZA WIZARA TATU MISITU YA HIFADHI

SHAKA AZITAKA TAASISI ZA UMMA NCHINI KUTENGA BAJETI ZA MIRADI

May 18, 2022
WIZARA YAANIKA MKAKATI MPYA KUKABILI BEI YA MBOLEA, MAFUTA

WIZARA YAANIKA MKAKATI MPYA KUKABILI BEI YA MBOLEA, MAFUTA

May 18, 2022
Instagram Youtube Twitter VK Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • 2021
  • Afya Makala
  • BURUDANI
  • Business
  • GAZETI LA BURUDANI
  • GAZETI LA UHURU
  • GAZETI LA UHURU MACHI 17
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • KIMATAIFA
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • RIWAYA
  • SIASA
  • Uncategorized

Recent News

TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

TAKUKURU YAIVALIA NJUGA MIRADI ILIYOKATALIWA MBIO ZA MWENGE

May 18, 2022
VIKUNDI VILIVYOPATA MIKOPO YA BILIONI 4/- VYAITWA TAKUKURU

VIKUNDI VILIVYOPATA MIKOPO YA BILIONI 4/- VYAITWA TAKUKURU

May 18, 2022

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In