WANAFUNZI wa kike katika Shule za Sekondari Wilayani Rorya Mkoani Mara wametakiwa kujitambua na kuwekeza muda mwingi katika masomo na sio kujiingiza katika vitendo vya anasa vinavyoweza kuwasababishia kukatisha masomo yao kutokana na mimba za utotoni.
Wito huo umetolewa wilayani huo na Mjumbe wa Baraza kuu la Wanawake Tanzania(UWT) Rhobi Samweli katika shule ya Sekondari Bukama pamoja na Nyamunga wakati wa ugawaji wa taulo za kike 242 zenye thamani ya shilingi Milioni Moja zilizotolewa na umoja huo Kwa watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu Wilayani humo.
Amesema ni vyema wanafanzi wa kike wakajitambua na kusoma kwa malengo na kuepukana na vishawishi toka kwa wanaume wasio watakia mema ili kujiepusha kujiingiza katika mahusiano katika umri mdogo na kuwa katika hatari ya kupata ujauzito pamoja na magonjwa kama vile ukimwi.
Nae mmoja ya wanafunzi Naomi Charles kutoka katika shule ya sekondari Bukama akiongea Mara baada ya kupokea msaada huo amesema taulo hizo zitawasaidia watoto wa kike wanaotoka Mazingira magumu kusoma Kwa kujiamini wanapokua katika hedhi kutokana na baadhi yao kushindwa kukaa darasani Kwa muda wote kutokana kukosa taulo za kujistili.
Kwa upande wake Afisa taaluma idara ya elimu sekondari wilayani Rorya Joyce Tongori amewataka wanafunzi hao kuweka bidii katika masomo yao na kuwataka kujiepusha na matumizi ya simu za Mkononi kwani muda huo haujafika.
Na Emmanuel Chibasa-Mara