VIJANA watakiwa kutumia talanta zao kama chachu ya kujipatia kipato na kuwaaminisha watu kuwa ni sehemu Moja ya kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza hayo Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malissa, amesema Vijana wengi wamekua na talanta mbalimbali hivyo kupitia Kampuni hiyo inaendeleza mchakato huo kuona Kwa jinsi gani vijana wanatimiza ndoto zao.
“Lengo la letu kuibua mashindano tofauti kwa ajili ya kukuza vipaji vya vijana, pia kukusanya vijana kupitia mtandao wa kijamii ili kupata washiriki katika shindano la ‘Bingwa Show’ mshindi akapatikana na kujinyakulia gari mpya, hivyo tuliona bado vijana wanahitaji vipindi ambavyo kwao itakua ni mchongo tukadondosha Tena shindano la ‘Mr right’.
“Kupitia talanta zao zinawawezesha kupata au kutimiza ndoto za maisha yao kumiliki gari za kifahari pamoja na fedha taslimu“ amesema.
Pia, Malissa ameongeza kuwa kwa kushirikiana na mchekeshaji maarufu nchini Coy Mzungu wameamua kuanzisha Shindano jipya liitwalo ‘The best comedy challenge’.
Aidha, Mkurugenzi wa Biashara na mikakati wa televisheni hiyo mpya, Isaya Kandonga, ameeleza namna alivyojikita zaidi katika maudhui ya Filamu za bongo na vipindi vya ‘Reality show’.
“Shindano la ‘The comedy challenge’ linakuja kuvunja mbavu za watu, hivyo naomba watanzania watazame na kutambua vipaji vya vijana kuona kijana anavyobadilisha maisha yake kupiti uwezo talanta aliyokuwa nayo,” amaesema.
Shindano hilo litaanza kuoneshwa rasmi Februari 6 kwa ajili ya kutoa burudani kwa watanzania.
Mchekeshaji Coy Mzungu, amefananua kuwa Startimes wanaendelea kuthamini vijana hivyo wachekeshaji hao watumie nafasi hiyo ya kujitangaza na kukamilsha ndoto zao.
“Fursa ya uchekeshaji ni miongoni mwa fursa zinazoleta kipato hivyo Kampuni hii imelibeba jukumu hilo na linaenda kuvabadilisha taswira na Mapinduzi katika tasnia hii kwa kupitia Shindano la “The best comedy challenge,”
Coy amefafanua zaidi kipengele kingine ni mchekeshaji anaependwa na watazamaji ataweza kujipatia shilingi Milioni 1 kama zawadi.
“Mshindi wa kwanza atajinyakulia gari aina ya “Crown” na mshindi wa pili atapatiwa pesa shilingi Milioni 5 huku mshindi wa tatu ataondoka na kitita shilingi milioni tatu kama kifuta jasho,” amasema.
Na AMINA KASHEBA