MAOFISA kutoka Idara ya Ardhi, Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, wamenusurika kufa baada ya wananchi wa Kijiji cha Melela, Kata ya Chita kuwashambulia na kuchoma moto gari la mkurugenzi wa hamalshauri hiyo.
Mbali na gari, watu hao pia wamechoma moto vifaa mbalimbali kikiwemo kinachotumika kwa upimaji ardhi chenye thamni ya sh. milioni 60.
Kutokana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatusi Muslimu, amesema watuhumiwa sita wanashikiliwa wakutuhumiwa kuhusika nalo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda Muslimu alisema tukio hilo lilitokea Agosti 6, mwaka huu saa 7.45 mchana katika Kitongoji cha Msondo kijijihi hapo.
Alisema kuwa kundi la watu waokadiriwa kuwa kati ya 15 hadi 20, walifi ka katika eneo hilo na kukuta maofi sa wakipima shamba lenye hekari 2,000 mali ya Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Balali ambaye kwa sasa ni marehemu.
Muslimu alisema Balali aliuziwa shamba hilo na kijiji mwaka 2001 kwa makubaliano ya kuwajengea zahanati, shule na huduma za maji ambapo mwekezaji huyo kwa zaidi ya miaka 20 hakutekeleza makubaliano hayo, ndipo ulipozuka mgogoro wa wananchi kutaka warejeshewe shamba hilo.
Alisema wananchi hao siku ya tukio walifi ka katika eneo ambalo maofi sa ardhi waliegesha gari na pikipiki tatu na kuamua kuchoma moto na kumjeruhi dereva wa gari hilo, Damas Sanga (51) sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo miguuni, kichwani na mkononi.
Alitaja vitu vilivyoteketezwa na moto huo ni gari aina ya Land Cruser lenye namba za DFP 9402, pikipiki tatu zenye namba za usajili Mc 282 AXS Sunlg, Mc 396 CUG Hojuo, Mc 327 BFR Tiberter pamoja na kompyuta mapakato tatu aina ya HP zenye thamani ya sh. milioni 7.2 na mashine ya kuhakiki mashamba, vyote mali za halmashauri.
Kutokana na tukio hilo, kamanda huyo alimtaka mtu mmoja mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Marashi anayemiliki hekari 400 ndani ya shamba hilo, kujisalimisha mara moja kituo cha polisi akituhumiwa kuchochea vurugu hizo.
Alisema watuhumiwa sita wanaoshikiliwa na polisi ni wafanyakazi wa Mrashi ambaye inadaiwa aliwatuma kufanya tukio hilo.
Baada ya tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigela alisitisha shughuli zote za upimaji kwa upande wa mwekezaji na wananchi kufanyika katika eneo hilo hadi hapo itakapoarifiwa.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Morogoro, Frank Mizakunte alisema shamba hilo lilikaa kwa muda mrefu bila ya bila ya kuendelezwa.
Alisema baada ya wananchi kuvamia, serikali ilitolea maelekezo kwa maofisa ardhi wa halmashauri ya Mlimba kwenda kuzungumza na wananchi na kukubaliwa hekari 500 zitolewe kwa kijiji na wananchi wakiwemo waliovamia.
Alisema kwa kuwa shamba lina hekari 2,000 na kwa kuwa wananchi ni wachache, hekari hizo 500 zitatumika pia kujenga miundombinu mingine kama shule na zahanati.
Hata hivyo, baadaye wananchi waliandika muhutasari kuomba kuvumiliwa kwani wapo waliolima ili wavune mazao yao.
Mizikunte alisema Agosti 5, mwaka huu maofi sa hao walikutana na viongozi wa kijiji na kukubaliana siku iliyofuata walianza kazi ya kupima, lakini wakiwa wanaendelea walijitokeza baadhi ya wananchi na kufanya vurugu.
Na LATIFA GANZEL, Morogoro