WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknologia Profesa Adolf Mkenda amesema ametenga muda wa wiki tatu kwa ajili ya kukaa ofisini, kukutana na wakuu wa Idara kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali huku akimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumuandalia nyaraka za kila Idara ili aweze kuzipitia kwa kina na kujifunza zaidi.
Pia amesema wizara ya Elimu ni wizara yenye mambo mengi ambayo haihitaji kuyachanganya changanya hivyo inahitaji umakini mkubwa katika bila hivyo watawachanganya watanzania.
Profesa. Mkenda ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi baina yake na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Profofesa. Joyce Ndalichako ambaye amehamishiwa wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu.
“Lazima nitenge muda maalum kwa ajili ya kujifunza zaidi, hivyo tatenga muda maalumu wa kupitia nyaraka muhimu za wizara hiyo kwa lengo la kufanya uchambuzi wa kuboresha elimu ya kitanzania kwa lengo la kuwa na elimu yenye tija, muda wote wakati najifunza naibu waziri wangu Jum Kipanga atakuwa akitekeleza majukumu mengine,”amesema.
Amesema ili waweze kuwa na maazimio ya pamoja na kutotoa matamko ambayo hayana azimio la pamoja kwani kauli ya waziri ya waziri ni kauli ya wizara na si ya familia hivyo lazima washirikiane na kufanya kazi bila woga.
“Wizara hii siyo ya kuchezea ni wizara nyeti sana na ukiichezea inahitaji na siyo kubadilisha badilisha mambo kwa kubadilisha mambo tutalichanganya taifa…..
“Tunataliwa kufanya kazi kama timu Mimi ni Waziri lakini hata pale ambapo naona kuwa kutakuwa na tatizo au nikaonekana kukomaa naomba nifuate niambie kuwa hapa panahitajika kufanyika jambo fulani” amesema Profofesa.Mkenda.
Pia amesema kuwa katika kuiboresha elimu ya kitanzania ambayo kwa sasa kumekuwa na ajenda katika mashaka ya ubora wake kwenye kikidhi mahitaji ya soko la ajira hataona shida kuwatafuta wataalamu wa elimu kukaa nao kwa nia ya kutoa mchango wao wa kuboresha elimu.
“lazima tuhakikishe tunawatafuta wataalamu wabobezi wa elimu hata kama ni wastaafu ili kuweza kupata mchango wao wa kuboresha elimu ya watanzania kwa manufaa ya taifa,”amesema.
Awali aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Profofesa.Joyce Ndalichako amesema kuwa wizara ya Elimu ina jumla ya taasisi 30 ikiwamo Baraza la mitihani Tanzania NECTA na Taasisi ya elimu Tanzania na nyinginezo.
Profesa. Joyce amesema wizara inatekeleza miradi mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi trioni 3 ukiwamo mradi wa lipa kulingana na matokeo ambao pia mradi unatarajiwa kuanza kutekelezwa kwa awamu ya pili katika kuboresha elimu ya Tanzania na miondombinu yake.
Pia amefafanua kuwa miongoni mwa miradi inayotekelezwa ni mradi wa kuimarisha elimu ya sekondari utakaogharimu zaidi ya shilingi trioni 1.15 utakaojenga shule 245 mpya zitakazokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 kila moja na ujenzi wa shule 26 za wasichana na wameanza na shule 10.
“Mradi mwingine kuwa ni wa kuimarisha elimu ya juu wa shilingi bilioni 982 umbao unatarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni utahusisha vyuo vikuu 14 pia mradi huo utahusisha kuwajengea uwezo wahadhiri kuondoa uhaba wa wahadhiri katika vyuo vikuu hapa nchini,”amesema.
Profesa. Joyce amesema kupitia fedha za UVIKO 19 zaidi ya shilingi bilioni 64 zimetumika katika ujenzi wa vyuo vya ufundi VETA katika Wilaya 25 na vyuo vya VETA vya mikoa 4 sambamba na kuhudumia watu wenye mahitaji maalumu kuhakikisha wanapata elimu na ujuzi wa kuwawezesha kujiajiri na kuwa na uwezo wa kujihudumia.
Amewashukuru watumishi wote wa wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliompa ambapo alisema yamkini kukaa kwake muda mrefu kwenye wizara hiyo ni kutokana na ushirikiano aliopewa na watumishi waliokuwa chini yake hali iliyosababisha mambo mengi kwenda vizuri.
“Niwashukuru sana watumishi wa wizara ya wlimu kwa ushirikiano mlionipa tulifanya kazi kama kikosi kimoja, kama familia moja bila kuchoka hata ilipolazimika kufanya kazi usiku na mchana mlifanya bila kujali, naomba vivyo hivyo mtoe ushirikiano kwa waziri Profesa Mkenda,”amesesitiza.
Na Happiness Mtweve, Dodoma